Top news
SEKTA BINAFSI ZINGATIENI KALENDA YA UFUNDISHAJI -PROF.MKENDA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewataka wawekezaji kwenye sekta ya elimu nchini kuzingatia kalenda ya ufundishaji ili kuepusha suala la kukaririsha watoto wanapojifunza madarasani.
.
"Na Sisi tunaanza kuona dalili hizo kwenye SAMIA SCHOLARSHIP tutakuja kupewa taarifa wangapi walipata SAMIA SCHOLARSHIP wameenda vyuo vikuu lakini wanashindwa kucopy" alisema.
.
Prof.Mkenda ameyasema hayo Aprili 11, 2025, alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 35 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo mkoani Morogoro.
.
Amesema kalenda hiyo imeandaliwa kwa kuhakikisha kwamba wakati wa kusoma kwa muda uliopangwa utamaliza kila kitu, na wanafunzi lazima wasome kwa masaa yale ya siku, sio kulazimishwa kukaa mpaka wanachelewa na wakati wa likizo kuwaambia msiende likizo, kaeni hapa.
.
Waziri Prof.Mkenda amesema mwenye mamlaka ya kutoa Kalenda ya ufundishaji ni Kamishna wa Elimu,na waraka wa Kamishna ni wa kimamlaka.
.
"Kuna wakati shule,zinaongeza muda wa kukaa shuleni wanafunzi kwa sababu pengine kuna uhaba wa walimu, kwahiyo ule muda wa kufunga shule wanafikiria ebu tuongeze muda kidogo ili tufidie masomo ambayo hayajafundishwa.
.
"Lakini kwa shule inayojitangaza kwamba wazazi hii ni shule yetu, ina walimu wa kutosha, walimu waliobora kabisa halafu wazazi wanaleta wanafunzi kwenye shule hiyo kwa ahadi hiyo, shule hiyo inaposhindwa kutokuwaachia wanafunzi kwenda likizo,inaonekana kuna kitu waliwadanganya wazazi hao" alisema Prof. Mkenda.
.
Aidha, Prof. Mkenda ametoa wito kwa watumishi wa wizara ya elimu kuzingatia majukumu yao ipasavyo.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

