WAZIRI MAJALIWA AMESEMA "AGIZO LA KUVUNJA KIKOSI KAZI BADO LIPO PALE PALE"
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema, "Agizo la kuvunja Kikosi Kazi lipo palepale, TRA walileta Vijana ambao hawajasomea kazi ya kodi, wamekuja Vijana ambao wana tamaa zao za Maisha, hapana, haikubaliki. Kodi zitakusanywa na Maafisa wa #TRA ambao wamesomea na wana Maadili ili wakikosea tuwabane"
.
Majaliwa Ameyasema Hayo Leo Mei 17,2023 Kwenye Kikao Na Wafanyabiashara Wa Soko La Kariakoo Kilichofanyika Katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
-
Ameongeza, "Tunajua Wafanyabiashara wana Mikopo, wanahitaji kupanua Biashara. Siku nne zilizopotea ni nyingi mno, nawaomba sana sana tuwarudishe Wafanyabishara walioondoka na kuhama Soko la Kariakoo"
@jamiiforums
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

