MIKOPO YA ELIMU YA JUU KUONGEZEKA 2025/26 KUFIKIA BILIONI 916-PROF.MKENDA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa shule mpya 103 za sekondari za amali.
.
"Kati ya shule hizo, shule 29 ni za amali za kihandisi na shule 74 ni za amali zisizo za kihandisi" alisema.
.
Prof. Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.
.
Aidha, Amesema mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka Kufikia Shilingi Bilioni 787.4 mwaka 2024/25 kutoka shilingi Bilioni 570 zilizotolewa mwaka 2021/22.
.
"Wanufaika wameongezeka kutoka Wanafunzi 177,925 mwaka 2021/22 hadi Wanafunzi 248,331 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 39.6" alisema Prof.Mkenda.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

