UJENZI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 CHAMWINO JIJINI DODOMA WAFIKIA ASILIMIA 48
Ujenzi wa Mradi wa maji wa Miji 28 Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma wenye gharama ya Tsh. Bilioni 17 umefikia asilimia 48 na jumla ya kiasi cha dola za kimarekani milioni moja na laki sita zimeshalipwa kwa mkandarasi kwenye mradi huu.
Mradi huu unatekelezwa chini ya Wizara ya Maji ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ni miongoni mwa wanufaika katika kanda yake ya Chamwino ambao unatekelezwa na Mkandarasi MEGHA Engineering & Infranstructures Limited (MEIL) kutoka nchini India.
Kazi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi wa matanki mawili ya lita laki mbili (200,000) eneo la Msanga, tanki la kuvunia maji la lita laki tano (500,000) katika eneo la Chamwino.
Pia ujenzi wa miundombinu ya kutibu maji na kituo kikuu cha kusukumia maji kwenda katika tanki la Buigiri lenye ujazo wa lita milioni mbili na laki tano (2,500,000) na tanki la juu mita 15 lenye ujazo wa lita laki mbili (200,000) katika kijiji cha Msanga.
Kazi nyingine zinazoendelea ni ulazaji wa mabomba kwa ajili ya usambazaji wa maji umbali wa kilometa 31 kwenda katika eneo la huduma yakitokea kwenye tanki la Buigiri maeneo ya Buigiri, Chinangali II, Mwegamile, Vikonje na Chamwino na usambazaji wa maji kutoka kwenye tanki la Msanga kwenda katika maeneo ya Kijiji cha Msanga.
Mradi huu unatarajiwa kumamilika tarehe 10 Desemba 2025, na kukamilika kwa mradi huu itasaidia kuboresha huduma na kuweza kusogeza huduma maeneo ya pembezoni kwa sababu mji wa Chamwino unakua kwa kasi kutokana na ongezeko la watu.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

