logo

TAASISI ZA SERIKALI IGENI MFANO WA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Ametoa Wito Kwa Taasisi za Serikali Kuendelea Kuiga Mfano Wa Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Kwa Kujitathimini, Na pia Kuona Namna Ambavyo wanafanya Kazi zao Vizuri ili Taasisi hizo zipate Muelekeo wa Namna Nzuri ya Kufanya Kazi Zao.

.

Majaliwa Ameyasema Hayo Leo Juni 05,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Maadhimisho Ya Miaka 5 Ya Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Na Akizindua Mafunzo Kwa Mawakili Wa Serikali Katika Ukumbi Wa Jakaya Kikwete Convertion Center.

.

Amesema Ni Ukweli Usiopingika Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali Ni Ya Kimkakati na Ina Dhamana Kubwa Katika Kuchangia ukuaji Wa Uchumi Wa Nchi Yetu kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

.

"Kwa Msingi Huo, Ofisi Hii Ni Nguzo ya Uwekezaji, Mazingira mazuri ya Biashara, Ukuaji Wa Sekta Ya Madini, Ujenzi na Upanuzi Wa Miundombinu kama vile Barabara, Reli ya Kisasa, Anga, Maliasili na Utalii. Na inategemewa Kuendesha Mashauri ya madai na Usuluhishi Kwa Wakati, Ufanisi Kwa muda mfupi na Kwa Kuzingatia Misingi ya Uadilifu na Uzalendo" Amesema Majaliwa.

.

Waziri Majaliwa Amesema Kutokana na Ukubwa Wa Majukumu ya Ofisi Hiyo,Ni jambo Jema Kufanya Tathmini ya Utendaji Kazi wao Ili kubaini Mafanikio na Changamoto walizonazo Katika Kipindi chote wanachoendelea kushika Dhamana Hiyo.

.

"Nimeelezwa Kuwa mnaendelea kuiwakilisha Serikali Vyema Katika Mashauri Mbalimbali na kama Hivyo ndivyo basi Tujipigie Makofi Sisi Wenyewe" Amesema Majaliwa.

.

Aidha, Majaliwa Amewataka Watendaji Wa Ofisi Hiyo Kuendelea Kufanya Kazi Kwa weledi Na waweke Maslahi ya Taifa mbele Na Serikali kwa Upande Wake Itaendelea kuwaunga Mkono.

.

Naye Waziri Wa Katiba Na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro Amesema Kwa Mwaka wa 2022/2023 Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali imefanikiwa kumaliza Mashauri 65, Na Kwenye Usuluhishi Mashauri 7 na Katika Mashauri hayo Yote wameweza kuiokolea Serikali Shiling Trilioni 7.57.

.

"Hiyo ni Kazi Nzuri ambayo inafanywa na Ofisi Ya Wakili Mkuu Wa Serikali ambapo Mimi Kama Waziri niliyekabidhiwa Dhamana kwenye Wizara Hii Ninaona Fahari Kuisema" Amesema Ndumbaro.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn