logo

NMB YAANDIKA HISTORIA,YATOA GAWIO LA BILIONI 45.5

BENKI Ya NMB Leo Juni 17,2023 imetoa gawio la Tsh.Bilioni 45.5, ikiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na Taasisi ya kifedha kwa Serikali.

.

Gawio hilo kwa serikali ni kiashiria tosha cha Azma yao ya kuhakikisha wanaleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wao wote, ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi - Dkt. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu - Ruth Zaipuna, wamemkabidhi Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya gawio hilo katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 25 ya mafanikio ya NMB Bank, inayoendelea katika ukumbi wa Mlimani CityDar es Salaam.

.

Tukio Hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba, Msajili Wa Hazina Ndg.Nehemia Mchechu, Waziri wa Fedha wa Serikali ya Zanzibar - Saada Mkuya Salum pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

@nmbtanzania

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn