RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yatakayofanyika Julai 10,2023 Jijini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri.
Akizungumza Leo Julai 08,2023 jijini Dodoma Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa kilele cha maadhimisho hayo Yataambatana na Gwaride la vijana wa JKT, Maonyesho mbalimbali ya vifaa vya SUMAJKT pamoja na burudani za ngoma kutoka katika vikundi vya JKT na wasanii mbalimbali.
“Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho haya atakuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan lakini pia kufuatia historia ya kuanzishwa kwa JKT na Nchi ya Israel tutakuwa pia na wageni kutoka Israel kupitia ubalozi wao Nchini Tanzania Pamoja na wageni wengine kupitia Chanel za Kidiplomasia” alisema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa pia ametoa wito kwa viongozi wote wa serikali, taasisi mbalimbali za Umma na binafsi, watumishi, wananchi wa mkoa wa Dodoma na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kilele cha maadhimisho hayo.
“Ninachukua fursa hii kuwaalika watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kilele cha maadhimisho haya siku ya Jumatatu kuanzia saa 12:30 Asubuhi katika viwanja vya Jamhuri, karibuni sana mumsikilize Rais na Amiri Jeshi mkuu” alisema.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

