logo

RAIS SAMIA AMESEMA "NCHI ZETU ZA AFRICA SIO VICHAKA VYA KUFUGA WALA RUSHWA"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Ametoa rai kwa wadau wote wa mapambano dhidi ya rushwa kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala haya ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano haya na kuchukua hatua muafaka.

.

Samia Ameyasema Hayo Leo Julai 11,2023 Alipokuwa Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya Mapambano dhidi Ya Rushwa Barani Africa yaliyofanyika Jijini Arusha.

.

Amesema wala rushwa wanapaswa kufahamu kwamba nchi zetu si vichaka vya kuficha fedha zilizotokana na rushwa au kufuga wala rushwa.

.

"Tunataka dunia nzima ifahamu kuwa, Afrika sio salama kwa wala rushwa, na hilo lionekane kwa vitendo kupitia hatua tunazozichukua dhidi ya wala rushwa na sio mikutano, makongamano na maneno peke yake" Amesema Samia.

.

Rais Samia Amesema Kwa mujibu wa Sheria Na.11 ya mwaka 2007, TAKUKURU imepewa majukumu ya kuhakikisha kwamba rushwa inatokomezwa Tanzania, na inafanya hivyo chini ya Kaulimbiu yake ya "Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu, Tutimize Wajibu Wetu.

.

"Pamoja na changamoto na dosari za hapa na pale, tumefanya na tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika matumizi ya fedha za umma na kuongeza uwazi ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa" Amesema Samia.

.

Aidha, Samia Amesema Maadhimisho hayo ni fursa muhimu inayotuwezesha kutafakari kwa kina, uwazi na kwa dhati kuhusu utekelezaji wa mkataba huo, tueleze mafanikio na changamoto zetu ili tupate njia bora za kutatua changamoto hizo.

.

Naye Waziri Wa Nchi,Ofisi Ya Rais, Menejimenti Ya Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene Amesema Pamoja Na Siku Ya Maadhimisho Hayo, Tutakuwa Tunaadhimisba miaka 20 ya Kazi ya Utekelezaji Wa Mkataba Wa Umoja Wa Africa Wa Kuzuia na Kupambana Na Rushwa.

.

Kwa Upande Wake Mkurugenzi Mkuu Wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni Amesema Maadhimisho Hayo yanatoa chachu ya Kutoa Elimu na Taarifa Katika Nyanja Mbalimbali Kuhusu Maadili,Utawala Bora,Dhana Ya Rushwa,Uhujumu Uchumi Nk.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn