logo

SIMBA TUMESAJILI VYUMA 3, LAZIMA BAHARI ITAPASUKA- TRY AGAIN

"KLABU ya Simba msimu huu imejizatiti kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mashindano yote tutakayoshiriki ndani na nje ya nchi. Mwaka huu unyama utakuwa mwingi.

.

Tumesajili, vyuma vitatu vimetua, vyuma vinavyokuja bahari itapasuka. Hivi karibuni mimi na Mohamed Dewji tumefanikisha kumsajili mchezaji mkubwa sana, kutoka klabu moja maarufu na hivi karibuni tutamtangaza.

"Naamini mchezaji huyo ataleta furaha kwa kushirikiana na wachezaji waliopo kuhakikisha Simba inakuwa bora. Hivyo nimshukuru sana Mohamed Dewji kwa kazi kubwa anayofanya. Mohamed Dewji anafanya kazi kubwa na jitihada zake ndio zimetufikisha hapa, yupo tena yupo sana na ataendelea kuwepo".

.

Mwenyekiti wa Bodi Ya Simba SC Ndg.Salim Abdallah ‘Try again’ Ameyasema Hayo Leo Julai 12,2023 Jijini Dar es Salaam alipokuwa Kwenye Hafla Ya Uzinduzi Wa Ushirikiano Baina ya Simba SC na Benki ya CRDB.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn