NMB YATUNUKIWA TUZO 3 ZA KIMATAIFA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki Ya NMB, Bi.Ruth Zaipuna Leo Agosti 02,2023 amezitambulisha rasmi tuzo tatu za kimataifa walizopewa katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi zao za Makao Makuu.
NMB imepokea Tuzo hizo kwenye Vipengele Tofauti Tofauti kama vile; Benki Bora Tanzania 2023 (Kutoka Tuzo za Umahiri za EuroMoney),Benki Bora ya Wateja Maalum (Kutoka Tuzo za Umahiri za EuroMoney) Na Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara (Kutoka Tuzo za Global Banking and Finance Review)
Tuzo hizo zimetolewa na majarida ya kimataifa yenye makao makuu yake London Nchini Uingereza.
.
NMB Hii inakuwa ni mara ya 10 kutambulika kama Benki Bora nchini ndani ya miaka 11 iliyopita huku ikidhihirisha ufanisi wao wa kiutendaji, mapinduzi ya kiteknolojia na ubunifu, uongozi dhabiti, na uimara wao katika kuleta masuluhisho yanayomgusa kila Mtanzania.
Aidha, NMB imetoa Shukrani Kwa wateja wao, wanahisa, wafanyakazi, Benki Kuu, Serikali pamoja na wadau wao wote kwa kuendelea kuwaamini na kuwafanya kuwa Benki Bora nchini.
@nmbtanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

