NMB YAINGIA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA NDEGE 'ATCL'
Benki ya NMB Leo Agosti 16,2023 imeingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo wateja wa shirika hilo wataweza kulipia tiketi za ndege kupitia mtandao wao mpana unaojumuisha Matawi 229, NMB Wakala zaidi ya 21,000 nchi nzima au kidijitali kupitia NMB Mkononi (USSD au App).
.
Hata hivyo,NMB kwa ushirikiano na kampuni ya Reliance Insurance, wateja wanaosafiri ndani ya nchi watakaokata tiketi kupitia Benki ya NMB, watapewa bima ya bure ikijumuisha, Bima maalum ya hadi Tsh 5,000,000 kwa ajili ya kifo au ulemavu wa kudumu utakaotokea wakati wa safari, Bima ya upotevu wa mabegi (Checked-In Baggage) - kiasi cha hadi TZS 300,000.
.
Na endapo safari itafutwa au kusogezwa mbele zaidi ya masaa 6, NMB imesema msafiri atalipwa hadi Tsh 150,000.
Huduma hiyo imezinduliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Bi.Ruth Zaipuna na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL,Mhandisi Ladislaus Matindi; na kushuhudiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Bw.Filbert Mponzi,Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL, Jamali Athuman Kiggundu na viongozi wengine kutoka taasisi zote mbili.
@nmbtanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

