Top news
WALIMU 42 KUTOKA KIGOMA, TABORA NA SONGWE KUPATIWA MAFUNZO NA UCSAF
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt.Wilson Charles amefungua mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Sekondari ambayo yameandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote( UCSAF), kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto Duniani (UNICEF).
Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma, pamoja na kuziunganisha na mtandao wa intaneti, ambapo walimu hupatiwa mafunzo ya matumizi ya vifaa hivyo kwa lengo la kuwawezesha kuvitumia katika ufundishaji.
Dkt.Charles ameipongeza UCSAF kwa kushirikiana na UNICEF kuratibu mafunzo hayo, ambayo amesema yatasaidia katika kuleta mapinduzi ya mbinu za ufundishaji hasa katika eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yaani TEHAMA.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF John Mukondya amesema, hadi sasa jumla ya walimu 3,465 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wamekwisha kupatiwa mafunzo hayo.
Jumla ya walimu 42 kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe watapatiwa mafunzo ambayo yanafanyika kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
@ucsaftz @uniceftz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

