logo

CRDB YACHANGIA MILIONI 20 UJENZI MARIAN SEC SCHOOL

BENKI ya CRDB kupitia Sera yake ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI Policy) imechangia Kiasi Cha Shilingi Milioni 20 Kwa Ajili Ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Marian inayojengwa pamoja na Zahanati,Katika eneo la Mlingotini, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.

.

Hayo Yamesemwa Na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Hiyo Bw.Abdulmajid Nsekela Alipokuwa akiongoza harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule Hiyo.

.

Katika Harambee Hiyo, Nsekela Yeye binafsi amechangia Shilingi milioni 10, na viongozi wengine waandamizi wa Benki ya CRDB walioambatana naye wakichangia zaidi ya Shilingi Milioni 10.

.

Harambee hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 26 tokea kuanzishwa kwa shule ya wasichana ya Marian.

.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Polycarp Pengo.

@crdbbankplc

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn