FANYENI VIZURI MASOMONI MTUPE HESHIMA -RIDHIWANI KIKWETE
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg.Ridhiwani Kikwete amewataka wanafunzi wa kidato cha sita shule ya kati ya Lugoba kuhakikisha wanafanya vizuri katika masomo yao ili wawape heshima jimboni hapo.
Ridhiwani Kikwete ameyasema hayo leo April 23,2024 alipokuwa akihutubia wahitimu wa kidato cha Sita katika shule ya Kati ya Lugoba,Halmashauri ya Chalinze.
Ndg.Kikwete amewahasa wahitimu hao kuhakikisha wanafaulu ili waache deni la kufuatwa na wadogo zao wanaowafuata kwa upande mmoja, wawape heshima Walimu na wazazi pia kwa kufaulu vizuri.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Sakasa ameishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka pesa za Elimu bure,vifaa na kuongezeka kwa madarasa na walimu shuleni hapo huku akimuomba Mgeni rasmi kuendelea kuikumbuka shule hiyo kwa kuisaidia vifaa na kuongeza mabweni ya wanafunzi.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

