logo

RAIS SAMIA AMEFANYA MENGI MAKUBWA YA MFANO,TUMUUNGE MKONO KWA VITENDO -DC FAKII LULANDALA

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Ndg.Fakii Raphael Lulandala amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya shughuli nyingi na kubwa na kuiletea Tanzania mafanikio makubwa ya Maendeleo katika sekta mbalimbali zote.

Lulandala ameyasema April 26,2024 alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa wilayani Simanjiro.

Amesema katika kipindi Cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imefanya mengi na makubwa katika jamii katika Sekta ya elimu kuna madarasa mengi yenye ubora mkubwa, kwenye Sekta ya afya karibia kila tarafa ina kituo cha afya, hospitali za wilaya na hospitali za mkoa.

"Tukisema tuorodheshe mambo mengi na makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka mitatu, muda hautatosha" alisema Lulandala.

Aidha,Lulandala amesema pamoja na kwamba bado kuna uhaba wa maji lakini mamlaka za maji zinafika mahali husika kupeleka maji pasipo changamoto yoyote ile.

Amesema wana Manyara wana furaha na wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuiendeleza,kudumisha na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Sisi kama wana Manyara tuna furaha kubwa sana na tunafunga mkono kabisa juhudi zinazofanywa na Serikali yetu katika kuiendeleza, kudumisha na kuimarisha Muungano wetu, pia tunaendelea kuwa wasimamizi Wazuri wa shughuli zote za miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa na kusimamiwa na Serikali hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ulinzi, Usalama Amani vinaendelea kuwepo miongoni mwa wananchi wetu" amefafanua

Lulandala.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi.Maryam Muhaji ameitaka jamii kuhakikisha wanaimarisha Muungano huo,pamoja na kukemea vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unaoendelea katika mkoa huo.

Kufuatia hayo,kuwepo kwa vitendo hivyo ndani ya Mkoa huo amewaomba viongozi wa dini katika makanisa na misikiti suala la ukatili wa Kijinsia iwe ndio agenda ya kukemea ukatili wa kijinsia.

"Wana Manyara ni wazuri sana isipokua lakini tunaharibiwa na huu ushetwani ambao umetutawala kwenye suala zima la Ukatili, hivyo viongozi wa Dini niwaombe kulitenda hili Kwa haraka zaidi ili liweze kuwa na mwitikio mzuri kwa jamii.

Aidha,Naye Katibu wa Siasa,Itikadi na Mafunzo Mkoa wa Manyara Bw.John Nzwalile amesema zipo faida nyingi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hivyo kuwaomba Watanzania kutoruhusu watu kuubeza Muungano huo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn