WAKUU WA MIKOA SIMAMIENI UTASHI WA RAIS SAMIA -WAZIRI MKUU MAJALIWA
WAZIRI Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa nchini waakisi utashi wa kisiasa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia na kutekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai.
.
Ametoa wito huo leo Jumatatu, Mei 6, 2024 wakati akifungua warsha ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya kuwajengea uelewa kuhusu maboresho kwenye mfumo wa Haki Jinai na utoaji wa haki nchini kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume Huru ya Uchaguzi, uliopo Njedengwa, nje kidogo ya Jiji la Dodoma.
.
Majaliwa amesema sambamba na suala la utashi, ni lazima viongozi na watendaji wa Serikali wawe na uelewa wa kutosha ili waweze kuyasimamia na kuyatekeleza mapendekezo hayo.
Amesema malalamiko ya wananchi katika masuala kadhaa ndiyo yaliyoweka msukumo kwa Mheshimiwa Rais kuunda Tume ya Haki Jinai na kuyakubali mapendekezo yaliyotolewa na Tume hiyo na hatimaye kuigeuza kuwa Kamati ya kuandaa mikakati utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.
.
Waziri Mkuu amesema utungaji wa baadhi ya sheria ndogo katika mamlaka zao ambazo aghalabu hukinzana na sheria mama.
“Mfano ni tozo zinazoanzishwa na halmashauri kama vile ushuru wa mabango, kodi za maegesho na usimamizi wa matumizi ya maeneo ya barabara zinasababisha mkanganyiko kwa wananchi kwa kuwajibishwa na chombo zaidi ya kimoja,” amesema.
Mapema, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt.Festo Dugange alisema kuwa ofisi hiyo itasimamia utekelezaji wa maagizo na maelekezo yatakayotolewa katika warsha hiyo ili dhamira ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuona wananchi wanapata haki zao inafikiwa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

