RAIS DKT.SAMIA AZINDUA MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA 2024 - 2034 JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameitaka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu kuandaa na kutoa katazo la matumizi ya nishati isiyo safi kwa taasisi zinazohudumia watu zaidi ya watu 100.
Rais Dkt.Samia ametoa agizo hilo leo Mei 8,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizindua Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia 2024 - 2034.
.
Amesema kuwa mkakati huo wa kitaifa pia utachangia jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kutokana na uharibifu wa misitu ambao huchangiwa na shughuli za kibinadamu ambapo inakadiriwa kuwa hekta 469,000 za misitu hupotea kutokana na matumizi ya mkaa na kuni.
.
Rais Samia ameziagiza Wizara, Taasisi, Mamlaka, wadau na sekta binafsi kuzingatia matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kulinda mazingira na athari nyingine zinazotokana na nishati isiyo safi.
.
Aidha, Rais Samia ameitaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuendelea kutekeleza jukumu lake la kusambaza nishati vijijini ikiwemo Nishati Safi ya Kupikia.
.
Naye, Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia kwa kuimarisha upatikanaji wa malighafi na raslimali za nishati hiyo.
“Mkakati huu ambao upo chini ya usimamizi wa Wizara ya Nishati na kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu utatakelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 4.6 umezingatia miongozo ya kitaifa na kimataifa”, amesema Majaliwa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko amesema kuwa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia yatasaidia wanawake na vijana kupata muda mwingi wa kufanya kazi sambamba na kulinda afya zao.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

