WAZIRI MKENDA KUZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA ELIMU,UJUZI NA UBUNIFU 2024 JIJINI TANGA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda anatarajia kuzindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 tarehe 27 Mwezi Mei, na yatahitimishwa rasmi mnamo tarehe 31 Mei,2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa.
.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo leo Mei 23,2024 alipokuwa akitoa taarifa ya Maonesho hayo jijini Dodoma ambapo amesema tukio hilo kubwa la Kitaifa litafanyika katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari ya Popatlal na ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Bahari Beach, Jijini Tanga, kuanzia tarehe 25 hadi 31 Mei, 2024.
.
"Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanaleta pamoja Taasisi, Mashirika, Wadau wa Maendeleo, Asasi, Watunga Sera, Wabunifu/Wagunduzi, na Wadau wengine, kutoka ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya mijadala na kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya elimu, ujuzi na ubunifu. Maadhimisho haya yanatoa pia fursa kwa watunga sera, wafadhili, wadau wa maendeleo, washirika wengine na umma kushuhudia tafiti, bunifu, teknolojia na bidhambalimbali." amesema Prof.Nombo.
.
Amesema Mashindano hayo yanatoa fursa kwa watafiti na wabunifu wachanga kukutana na wawekezaji wanaoweza kuchangia katika kuendeleza na kubiasharisha bunifu na teknolojia zao.
.
Aidha, Prof.Nombo amesema katika maonesho hayo kutakuwa na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), Mashindano ya ujuzi (Skills Competition)kwa wanafunzi wa Vyuo vya Ufundi na Ufundi Stadi nk.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

