logo

RAIS SAMIA KUZINDUA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 JANUARY 31,2025 JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023 na Mitaala iliyoboreshwa.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma Januari 31,2025 ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewaalika watanzania wote katika uzinduzi huo wa Kihistoria.

.

Prof.Mkenda amesema sambamba na sera, mitaala nayo imefanyiwa mapitio na kubadilishwa kuendana na sera ambayo tunayo, hivyo kwa hivi tuna mitaala mipya ambayo wanaitekeleza kwa awamu.

.

"Suala hili ni kubwa, mageuzi yaliyopo kwenye elimu ni makubwa sana na yataanza kutekelezwa kwa awamu huku watu wakiwa wanaona Kila mwaka,hatua ambazo zinachukuliwa.

.

"Ni mabadiliko ambayo yatagusa vizazi mpaka vizazi ukamilifu wa utekelezaji wake kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha sita utachukua muda,kwa Sababu tulianza hatua kwa hatua" alisema Prof.Mkenda.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn